>

MERIDIANBET WAANZISHA SHINDANO LA MIKWAJU YA PENATI KUISAIDIA JAMII

Meridianbet inaendesha shindano la upigaji wa mikwaju yake penati kwa ajili kuchangisha fedha ambazo lengo la ukusanyaji wa fedha hizo likiwa ni kurejesha kwa Jamii. Kampuni hii ambayo ni wakongwe na magwiji wa ubashiri wa michezo na kasino ya mtandaoni, wamekuwa wakifanya shughuli mbali kama hizi zinazowaweka karibu zaidi na Jamii.

Wakati huu Kampuni imeamua kuwatumia watu maarufu na wahamasishaji kuichangia Jamii, ambapo mashuti ya penati yanatoa thamani ya mchango ambao mtu huyu anayepiga anaisaidia Meridianbet kuichangia Jamii. Kila shuti linalofikia nyavu limepewa thamani ya TSH 50,000. Baada ya kushinda mashuti kadhaa kati ya mikwaju mitano anayotakiwa kupiga, mhamasishaji anachagua kundi gani la jamii lisaidiwe kwa fedha hizo.

Wakiwa na balozi wao, na mhamasishaji Jemedari Saidi Kazumari aliyepiga penati 5 na kupata 4 kati ya hizo na kufanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi laki 200,000/=. Jemedari alipendekeza fedha hizi zipelekwe kwenye taasisi ya tiba ya CCBRT.

Meridianbet iliwasilisha fedha hizo CCBRT, ambao walitoa utaratibu sahihi wa kupekela kiasi kile kwa walengwa ambao ni watu wanaohitaji huduma za kitabibu hospitalini hapo.

Uongozi wa CCBRT ulielekeza kiasi hicho kwenye matibabu ya mtoto Agness Elias aliyepaswa kufanyiwa upasuaji wa miguu ambao gharama za upasuaji na matibabu ya kiasi cha 250,000/=.