JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union amesema kuwa wanatambua kwamba leo wana mchezo mgumu wa fainali dhidi ya Yanga lakini wachezaji wake wanajua nini ambacho wanahitaji.
Coastal Union ilitinga hatua hii kwa ushindi mbele ya Azam FC kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Coastal Union ilishinda kwa penalti 7-6 Azam FC na kutinga fainali huku ikikutana na Yanga iliyoshinda kwa bao 1-0 dhidi ya Simba.
“Kikubwa ni kwa wachezaji wetu kuweza kupata matokeo na hilo lipo kwetu,hatua ambayo tumefika sio mbaya hivyo mashabiki wawe pamoja nasi kwani wamekuwa nasi tangu awali.
“Uzuri ni kwamba wote tunaingia kwenye mchezo kushindana hivyo siwezi kusema ninatuma salamu kwa wapinzani wangu ama ninafanya nini hapana tunakwenda kushindana ili kupata matokeo,” amesema.
Inakuwa ni mara ya tatu kwa Coastal Union kumenyana na Yanga msimu huu kwa kuwa ilikutana na timu hiyo mara mbili kwenye ligi na mechi zote Coastal Union ilipoteza.