RASMI mabosi wa Singida Big Stars wameweza kumtambulisha nyota mpya katika kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao.
Anaitwa Aziz Andambwile ambaye alikuwa akitajwa kuwaniwa pia na Klabu ya Namungo inayotumia Uwanja wa Ilulu.
Ni kiungo mwenye uwezo wa kucheza nafasi tofauti tofauti uwanjani. Mchezaji kijana, mzawa, msomi, mpambanaji wa kweli akiwa na timu yake mpaka timu ya Mbeya City na Timu ya Taifa ya Tanzania,Taifa Stars.
Nyota huyo ameshacheza Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na timu ya Big Bullet ya Malawi.