MRITHI MIKOBA YA JOHN BOCCO KUJULIKANA

ILE vita ya nani atasepa na kiatu cha ufungaji bora kilicho mikononi mwa John Bocco nahodha wa Simba itajulikana rasmi leo Juni 29,2022 kwenye mechi za mwisho wa msimu wa ligi.

Mpaka sasa hakuna mwenye uhakika wa kusepa na kiatu hicho kati ya washambuliaji wawili ambao ni mzawa Geogrge Mpole wa Geita Gold pamoja na Fiston Mayele kutoka DR Congo nyota wa Yanga.

Mastaa hawa wawili wote msimu huu wametupia mabao 16 huku Mpole akiwa ametoa pasi tatu wakati Mayele akiwa nazo tano kibindoni.

Ikumbukwe kwamba mfungaji bora wa msimu uliopita alikuwa ni Bocco ambaye alitupia mabao 16 na kutoa pasi mbili za mabao na msimu huu ametupia mabao matatu.

Juni 29,wakali hawa wa kucheka na nyavu watakuwa kazini ambapo Mpole wa Geita Gold timu yake itamenyana na Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani,Tanga na Mayele timu ya Yanga itamenyana na Mtibwa Sugar,Uwanja wa Mkapa.