MSIMU wa 2021/22 umekamilika ambapo mbivu na mbichi zimejulikana.
Biashara United ya Mara itacheza Champioship msimu ujao ikiungana na Mbeya Kwanza ya Mbeya.
Mtibwa Sugar wao watacheza mtoano na Tanzania Prisons ili kusaka timu itakayobaki ndani ya ligi.
Matokeo yapo namna hii:- Kagera 0-0 Polisi Tanzania. Mbeya Kwanza 0-0 Simba,
Yanga 1-0 Mtibwa mtupiaji ni Dennis Nkane dk ya 80
Dodoma Jiji 1-0 KMC mtupiaji ni Wazir Jr dk12.
Ruvu Shooting 1-0 Tanzania Prisons, Fullu Maganga dk 10
Coastal Union 1-1 Geita Gold Chambo dk 20 kwa Coastal Union na George Mpole dk10.
Mbeya City 1-1 Namungo ni Ssemujju alitupia dk ya 47’ kwa Mbeya City,Sixtus Sabilo dk 17.
Azam 4-1 Biashara ni mabao ya Mbombo dk 13 kwa mkwaju wa p, dk 46, dk 64 na Tigere 79 huku lile la Biashara likifungwa na Kabeja 72.