KIUNGO WA KAZI SIMBA APEWA MKATABA

KIUNGO wa kazi ngumu ndani ya kikosi cha Simba SC, Mzamiru Yassin, amejifunga miaka miwili kuendelea kuvaa uzi mwekundu.

Mzamiru ni chaguo la kwanza la Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Seleman Matola ambaye amempa jukumu la kuichezesha timu na kusambaza mipira mirefu kama alivyofanya kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Mbeya City.

Mzamiru ambaye alijiunga na Simba mwaka 2015 akitokea Mtibwa Sugar, atakuwepo hapo mpaka 2024 baada ya kuongeza mkataba hivi karibuni.

Habari zimeeleza kuwa “Mzamiru amepewa mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kukipiga Simba, hiyo ni baada ya kazi yake kueleweka.

“Bado yupo ndani ya Sima hivyo wale ambao walikuwa wanahitaji saini yake wana kazi ya kuweza kuvunja mkataba na mabosi wa Simba.”

Msimu huu Mzamiru kafunga mabao mawili na kutoa pasi mbili za mabao.