Home Sports KICHUYA AWEKA REKODI YAKE BONGO

KICHUYA AWEKA REKODI YAKE BONGO

SHIZA Ramadhan Kichuya staa wa Namungo jana amefunga mabao matatu kwenye mchezo wa ligi na kufanya aweze kufunga hat trick kwenye mchezo huo ikiwa ni ya pili ndani ya ligi.

Kichuya alifunga mabao hayo ilikuwa dk ya 23,50 kwa mkwaju wa penalti na lile la tatu ilikuwa dk ya 66 kwenye ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Manungu.

Bao lingine la Namungo lilifungwa na Sixtus Sabilo dk ya 74, Mtibwa Sugar wao mabao yao yalifungwa na Nzigamasabo Stve dk ya 5 kwa mkwaju wa penalti na moja lilifungwa na George Makang’a dk ya 10.

Kwa msimu wa 2021/22 ni Jeremia Juma wa Tanzania Prisons alikuwa wa kwanza kufunga hat trick msimu huu ilikuwa mbele ya Namungo kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela.

Ni mzunguko wa 29 umeweza kumpata staa mwingine ambaye ameweza kufunga hat trick ndani ya ligi na wote wakiwa ni wazawa.

Previous articleVIDEO:SIMBA YAFUNGUKIA ISHU YA MORRISON,MASHABIKI
Next articleMWAMBA HUYU HAPA ANATUA YANGA,NDANI YA SPOTI XTRA JUMANNE