WAPE TABASAMU KUFANYIKA UWANJA WA SABASABA,MORO

ANAANDIKA Dickson Job,beki wa kikosi cha Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania,Taifa Starsnamna hii:-Habari watanzania. Mimi ni DICKSON JOB mchezaji wa Klabu ya Yanga. Nawakaribisha kutuunga mkono Katika siku maalumu tuliyoiandaa kwaajili ya kutoa Shukran zetu kwa jamii tuliyoipa jina la WAPE TABASAMU itakayofanyika tarehe 08/07/2022 Mkoani Morogoro.

Siku hii ni maalumu kwaajili ya kuwafariji watoto yatima wanaoishi Katika vituo mbalimbali mkoani MOROGORO pamoja na kutoa msaada kidogo kwa wamama wajawazito wanaohudumiwa katika Hospitali ya mkoa Morogoro.

Pia kutakuwa na mchezo wa hisani Kati ya TEAM JOB vs TEAM KIBWANA utakaokuwa ni mahususi kwa kuchangisha fedha kwaajili ya mahitaji ya watoto hao.

Mchezo huu utafanyika katika Uwanja wa Sabasaba,Moro kwa kiingilio cha sh 1,000 tu.

Tunawakaribisha wote watakaoguswa kuungana na sisi kwa chochote kile watakachobarikiwa.
Namba: 0716678781
Jina: Seif Hamisi

WAPE TABASAMU WAFARIJIKE.