MAKOCHA HAWA WAINGIA RADA ZA SIMBA

TARIK Sektioui ambaye aliwahi kuifundisha RS Berkane ya Morocco ni raia pia wa Morocco anatajwa kuwa kwenye mazungumzo na Simba.

Kocha huyu anatajwa kuwa miongoni mwa warithi wa Pablo Franco ambaye alifutwa kazi baada ya kupoteza mchezo wa Kombe la Shirikisho mbele ya Yanga.

Kwa sasa timu hiyo ipo chini ya Kaimu Kocha Mkuu ambaye ni mzawa Seleman Matola,ameongoza kwenye mechi mbili za ligi ambazo ameshinda zote ilikuwa mbele ya Mbeya City na KMC.

Pia kocha mwingine ambaye anatajwa kuwa kwenye rada za Simba ni Jozef Vukusic raia wa Slovakia.