MABEKI WA KAZI WAWILI KUPEWA MIKATABA YANGA

MABEKI wa kazi ndani ya Yanga, Djuma Shaban na Yannick Bangala wapo kwenye mazungumzo na mabosi wao ili kuweza kuongeza kandarasi kwa ajili ya kuendelea kutimiza majukumu ndani ya timu hiyo.

Nyota hao wote wawili mwaka 2021 walisaini dili la miaka miwili kutumikia uzi wa Yanga na sasa dili lao limebakisha mwaka mmoja.

Mabosi wa Yanga wanatajwa kuzungumza na meneja wa wachezaji hao ili waweze kuona namna ya kuweza kuboresha mikataba ya wachezaji hao.

Wote wawili wamekuwa ni tegemeo kikosi cha kwanza cha Nasreddine Nabi ambapo Djuma ni kinara wa kutoa pasi za mwisho akiwa nazo tano huku Bangala ukuta wake ukiwa umeruhusu mabao machache ya kufungwa ambayo ni 7.

Meneja wa wachezaji hao anaitwa Faustino Mukandila anatajwa kuja Bongo kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Yanga.

Haji Manara, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa hawataruhusu mchezaji wanayemhitaji kuweza kuondoka ndani ya timu hiyo.