KOCHA mpya wa Manchester United, Erick ten Hag anatajwa kuwa kwenye hesabu za kumsajili Frenkie de Jong kwa ajili ya kuwa naye kwenye kikosi msimu ujao.
Kocha huyo anamuamini kiungo huyo Mholanzi akiamini kwamba atakuwa bora kwenye mfumo wake akimpeleka pale Old Trafford.
Ten Hag hataki klabu hiyo imwage fedha kwa wachezaji ambao hawapi kipaumbele sana kama Christian Eriksen.
De Jong atakaposajilwa kutoka Klabu ya Barcelona ndipo kocha huyo ataamua nani atafuata kusajiliwa kwenye bajeti ambayo itakuwa imebaki.