BWALYA: NITAIMISI SIMBA, NAWAPENDA MASHABIKI WA HII TIMU

KIUNGO wa kimataifa wa Zambia, Rally Bwalya, juzi Jumapili alicheza mchezo wa mwisho dhidi ya KMC wa Ligi Kuu Bara akiwa Simba baada ya kuitumikia kwa kipindi cha misimu miwili.

Bwalya alijiunga na Simba Agosti 2020 akitokea Power Dynamos ya Zambia akisaini mkataba wa miaka mitatu. Katika mchezo wa juzi uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar, Simba ilishinda 3-1.

Kiungo huyo anaondoka Simba akiwa amebakiwa na mkataba wa mwaka mmoja baada ya Amazulu ya Afrika Kusini kufanikiwa kumsajili.

Baada ya mchezo huo, Bwalya alisema: “Mchezo wa mwisho. Nalazimika kusema kwa heri kwa watu wangu wote ninaowapenda.

“Siku yangu ya mwisho kama mchezaji wa Simba SC imekuwa ya hisia kubwa sana, asante kwa kuniaga kwa ushindi. Ninathamini mapenzi, bila shaka nitawamisi kila siku. Asanteni sana.”