KOCHA AFUNGUKIA KASI YA MPOLE

FELIX Minziro, Kocha Mkuu wa Geita Gold amesema kuwa bado anaamini kwamba mshambuliaji wake George Mpole ataendelea kutimiza majukumu yake ya kufunga pale anapopata nafasi.

Mpole ni namba moja kwa utupiaji kwa wazawa akiwa na mabao 15 na pasi tatu za mabao ndani ya ligi huku Fiston Mayele wa Yanga akiwa ni kinara wa utupiaji ana mabao 16 na pasi tatu za mabao.

Minziro amesema kuwa wachezaji wake wote wapo tayari kwa ajili ya mechi zao na kikubwa ni kupata ushindi.

“Ugumu wa kupata pointi tatu kwenye mechi tunazocheza ni mkubwa hivyo wachezaji wote ikiwa ni pamoja na mshambuliaji Mpole,(George) bado wana kazi ya kufanya kufunga mabao zaidi.

“Unajua ili uweze kupata ushindi ni lazima ufunge kwa maana hiyo hiyo ni kazi ya wachezaji wote na huwa tunafanyia kazi kwenye uwanja wa mazoezi kwa kuwapa mbinu za kufanya wachezaji,” amesema Minziro.

Mpole ana mabao 16 sawa na Mayele akiwa ni mzawa wa kwanza kwa utupiaji ndani ya ligi