WAKATI kasi ya Biashara United ikizidi kupunguzwa kwenye spidi ya kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2022/23 mmoja ya watupiaji alikuwa ni George Mpole.
Kwenye mchezo uliochezwa jana, Uwanja wa Nyankumbu, ubao ulisoma Geita Gold 2-0 Biashara United ikiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili.
Mabao ya Geita Gold yalipachikwa na Mpole dk ya 30 na lile la pili lilipachikwa na Edmund John ilikuwa dk ya 66 na kuwafanya Biashara United kuyeyusha pointi tatu mazima.
Kwenye msimamo sasa inakuwa nafasi ya 15 pointi 25 baada ya kucheza mechi 28 huku Geita Gold wakirejea nafasi ya tatu na pointi zao ni 42 baada ya kucheza mechi 28.
Mpole anakuwa ni mzawa namba moja kwa utupiaji kibindoni ana mabao 16 msimu wa 2021/22 huku kwa wageni akiwa ni Fiston Mayele wa Yanga kutoka DR Congo mwenye mabao 16 pia