KWENYE mchezo wa leo wa NIFUATE wa SAMAKIBA Foundation,Team Kiba wameibuka mabingwa kwa ushindi wa penalti 4-2 dhidi ya Team Samatta baada ya dk 90 kutoshana nguvu kwa kufungana mabao 3-3.
Mabao ya Team Kiba yalifungwa na Simon Msuva ambaye alitupia mawili dk ya 23 na 67 huku moja likifungwa na Alikiba kwa penalti dk ya 60.
Kwa upande wa Team Samatta ni mabao ya Kelvin John dk ya 42,Mbwana Samatta dk ya 77 na Idd Gambo dk ya 87 kwa mkwaju wa penalti, Uwanja wa Mkapa.
Mapato yaliyopatikana uwanjani ni kwa ajili ya kuweza kupeleka kwenye msaada sehemu ambayo wataamua iwe hivyo,hongereni SAMAKIBA Foundation,mashabiki kwa jambo hili kubwa.
Haji Manara alikuwa ni msemaji wa pande zote mbili kwa Timu Samatta na Timu Kiba ambapo wakati mchezo ukiendelea leo aliweza kuibuka katikati ya uwanja na kuanza kupiga stori na mwamuzi wa kati huku akionekana kulalamika.
Mzee wa kutetema Fiston Mayele yeye alikuwa miongoni mwa nyota ambao wamecheza upande wa Timu Kiba lakini hakuweza kutupia kwenye mchezo wa leo.