MPANGO WA BIASHARA WAKWAMA KAITABA

MPANGO wa Biashara United kusepa na pointi tatu mbele ya Kagera Sugar ulikwama baada ya kushindwa kushinda.

Huo ulikuwa ni mchezo wa kwanza wa Kocha Mkuu, Khald Adam ambaye alichukua mikoba ya Vivier Bahati ambaye alifutwa kazi kutokana na mwendo mbaya wa timu hiyo kwenye mechi 6 mfululizo.

Kagera Sugar nao wakiwa Uwanja wa Kaitaba walikwama kuvuna pointi tatu aada ya ubao kusoma Kagera Sugar 0-0 Biashara United.

Biashara United inafikisha pointi 25 ikiwa nafasi ya 15 baada ya kucheza mechi 27 huku Kagera Sugar ikiwa nafasi ya 7 na pointi 34.