WATATU WA YANGA KUIKOSA COASTAL UNION

MASTAA watatu wa Yanga wanatarajiwa kuukosa mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Juni 14,2022.

Diarra Djigui kipa namba moja wa Yanga anatarajiwa kuukosa mchezo wa ligi dhidi ya Coastal Union.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, kesho Jumatano saa 2:30 usiku ukiwa ni wa mzunguko wa pili.

Sababu kubwa ambayo itamfanya aweze kuukosa mchezo huo ni kutokana kuweza kufanya mazoezi na timu mara moja kwani alikuwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa ya Mali.

Mwingine ni nahodha na beki wa kati Bakari Mwamnyeto yeye ni majeruhi hivyo bado hajawa fiti.

Beki wa kazi Kibwana Shomari yeye ana kadi tatu za njano kwa hivyo ataukosa mchezo wa kesho ni kwa mujibu wa Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

Katika mzunguko wa kwanza Yanga ilishinda kwa mabao 2-0 Uwanja wa Mkwakwani hivyo kesho watahitaji ushindi ili kuweza kufanikisha lengo la kutwaa ubingwa wa ligi.

Ikiwa itashinda mchezo wa kesho itafikisha pointi 67 ambazo hazitafikiwa na timu yoyote ndani ya ligi msimu huu.