PUMZIKA KWA AMANI DAMIANO KOLA MZAZI WA RODGERS WA AZAM

JANA Juni 12,2022 ilikuwa ni safari ya mwisho duniani ya baba mzazi wa mashambuliaji wa Azam FC, Rodgers Kola aitwaye Damiano Kola Senior.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu, mahala pema peponi. Amen.

Taarifa ya kutangulia kwa haki kwa mzazi huyo wa Kola ilitolewa na Azam FC Juni 10,2022.

Msimu huu mshambuliaji huyo amekuwa kwenye ubora wake amapo ni namba moja kwa utupiaji ndani ya kikosi cha Azam FC.

Katupia jumla ya mabao 9 na mchezo wa mwisho kupachika bao la 9 ilikuwa mbele ya Ruvu Shooting ambapo alifunga bao hilo akitokea benchi.