KOCHA WA AL AHLY YA MISRI ABWAGA MANYANGA

KLABU ya Al Ahly ya Misri imefikia makubaliano ya kuachana na Pitso Mosimane ambaye alikuwa ni Kocha Mkuu wa timu hiyo ya Misri.

Hatua hiyo ya kuachana na Al Ahly ni maamuzi ya Pitso mwenyewe baada ya kikao na bodi ya wakurugenzi ya Klabu ya Al Ahly ambayo ni moja ya timu kubwa na bora ndani ya bara la Afrika.

Rais wa Klabu ya Al Ahly,Mahmoud El Khatib alikuwa kwenye kikao cha maamuzi hayo pamoja na Yassin Mansour ambaye ni Mwenyekiti wa Al Ahly, Hossam Ghaly mjumbe wa bodi ya timu pamoja na mipango ya timu kuweza kujadili hatma ya Mosimane.

Kutokana na kikao hicho taarifa imeeleza kuwa walikubali kwa pamoja kuendelea kufanya kazi na kocha huyo kutokana na mafanikio ambayo ameweza kuipa timu hiyo ikiwa ni pamoja na ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Lakini kocha mwenyewe ameomba kuondoka ndani ya kikosi hicho na kwa mafanikio ambayo amewapa ameona kwamba inatosha.

Ikumbukwe kwamba msimu huu Al Ahly imeishia hatua ya fainali na kupoteza mbele ya Waydad kwa kufungwa bao 1-0 ilikuwa ni Mei 30,2022.

Na Dizo Click.