MASTAA HAWA 11 WANASEPA NDANI YA MANCHESTER UNITED

KLABU ya Manchester United, imethibitisha kuondoka kwa nyota wake 11, kati ya hao yupo Paul Pogba na Jesse Lingard.

Wachezaji hao wanaondoka kwa sababu tofauti ikiwemo mikataba yao kumalizika na wengine kustaafu kucheza soka.

Edinson Cavani, Paul Pogba, Nemanja Matic, Jesse Lingard na Juan Mata, wanaondoka
baada ya mikataba yao kumalizika.

Kipa Lee Grant, yeye amestaafu soka na sasa anaenda kuwa Kocha wa Ipswich Town akisaidiana na nyota wa zamani wa United, Kieran McKenna.

Kwa upande wa wachezaji watano wa akademi, wanaotajwa kuondoka ni D’Mani Mellor, Reece Devine, Connor Stanle na kipa Paul Woolston ambaye amelazimika kustaafu akiwa na umri mdogo kutokana na kuandamwa na majeraha ya mara kwa mara.

Manchester United imethibitisha wachezaji hao kuondoka, huku wengine wanaotajwa kuwa njiani kuondoka ni Anthony Martial, Eric Bailly, Phil Jones na Axel Tuanzebe.

Hata hivyo, United kwa sasa pia ina mpango wa kumuuza beki wake Aaron Wan-Bissaka kurudi timu yake ya zamani ya Crystal Palace, huku Dean Henderson pia akitaka kuondoka.