KMC HESABU ZAO ZA MZUNGUKO WA PILI ACHA KABISA

UONGOZI wa KMC umeweka wazi kwamba kwa sasa hesabu zao ni kuweza kufanya vizuri mechi zilizopo mbele yao katika kumaliza mzunguko wa pili.

Baada ya kucheza mechi 25 KMC imekusanya pointi 31 ipo nafasi ya 10 kwenye msimamo.

Mchezo wao ujao ni dhidi ya Tanzania Prisons iliyo nafasi ya 14 na pointi 25 inapambana kujinasua kutoka mstari wa kushuka daraja.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa KMC,Christina Mwagala amesema kuwa mechi zote zijazo za mzunguko wa pili ni muhimu na wanahitaji kushinda.

“Kwa mechi za mzunguko wa pili kwetu itakuwa ni kazi kubwa kusaka pointi tatu na benchi la ufundi linakamilisha mipango kazi ili kuweza kupata matokeo,” amesema.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Juni 14, Uwanja wa Tanzania Prisons.