YANGA YAPIGA 8-0 FRIENDS RANGERS

KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi jana kiliibuka na ushindi wa mabao 8-0 Friends Rangers katika mchezo wa kirafiki.

Mabao ya Yanga yalifungwa na kiungo Dennis Nkane ambaye alitupia kamba mbili, Fiston Mayele alitupia kambani mara moja mzee wa kuwajaza Heritier Makambo yeye alitupia kamba mbili.

Mshambuliaji chipukizi wa timu hiyo Yusuph Athuman yeye alicheka na nyavu mara tatu kwenye mchezo huo wa kirafiki.

Yanga ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 64 baada ya kucheza mechi 26