MPANGO WA YANGA NI KUJA KIVINGINE MSIMU UJAO

 HAJI Manara, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa msimu ujao watakuja kwa sura mpya kwenye mashindano ambayo watashiriki pamoja na ligi kwa kufanya usajili makini.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 64 baada ya kucheza mechi 26.

Manara amesema kuwa wanatambua ushindani utakuwa mkubwa hivyo nao watakuja kwa ukubwa zaidi.

“Kwetu sisi tunahitaji kuona msimu ujao tunakuwa tofauti zaidi na kufanya usajili mkubwa ambao utatufanya tuwe katika utofauti kwa msimu mpya kitaifa na kimataifa.

“Tunachokifanya kila mechi tunaichukulia kwa umakini mkubwa na kwa namna ambavyo tumepanga kufanya usajili mkubwa itatupa nguvu sisi kufanya vizuri kimataifa,” amesema Manara.