KIKOSI cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars jana jioni Alhamisi ya Juni 2 kilikwea pipa kuelekea nchini Benini kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa kuwania kufuzu Afcon 2023 dhidi ya Niger unaotarajiwa kuchezwa kesho Juni 4.
Leo Juni 3 tayari kimewasili salama Benin ambapo mchezo huo utachezwa.
Benchi la ufundi limeweka wazi kwamba wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo muhimu na ambacho wanahitaji ni ushindi.
Stars ipo kwenye Kundi F ambapo kibarua chao wataanza dhidi ya Niger kesho kisha watarejea kwa ajili ya mchezo dhidi ya Algeria utakaopigwa Juni 8,mwaka huu 2022.
Kocha Mkuu wa Stars, Kim Poulsen amesema kuwa wanajua mchezo utakuwa mgumu lakini wapo tayari kuweza kufanya vizuri.
“Tunajua kwamba mchezo utakuwa mgumu kutokana na ukweli kwamba tunakwenda kucheza nje ya nyumbani licha ya kwamba mchezo unachezwa Benin,lakini tunajiamini na maandalizi ambayo tumeyafanya tunapaswa kuanza kwa ushindi,” amesema