KIKOSI cha Simba kimepoteza mchezo wa hatua ya nusu fainali mbele ya Yanga kwa kufungwa bao 1-0 uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.
Pablo Franco ameongoza kikosi chake ndani ya dakika 90 na kushuhudia wakishindwa kupata ushindi.
Bao pekee la ushind kwa Yanga limefungwa na Feisal Salum ilikuwa dk ya 25 kwa shuti kali akiwa nje ya 18.
Sasa Yanga inakwenda fainali itakutana na mshindi wa mchezo kati ya Coastal Union ama Azam FC ambao utachezwa kesho.