STAA wa Tottenham Son Heung-min ameweza kuweka rekodi yake ndani ya Ligi Kuu England baada ya kutwaa tuzo ya kiatu cha ufungaji bora alipoweza kufikisha mabao 23.
Nyota huyo anakuwa raia wa kwanza kutoka bara la Asia kuweza kutwaa tuzo ya ufungaji bora ndani ya Ligi Kuu England iliyoisha msimu wa 2021/22 alipoweza kufikisha mabao 23.
Pia nyota mwingine ambaye naye alitwaa tuzo hiyo ni raia wa Misri, Mohamed Salah ambaye naye alifunga pia mabao 23 na yeye anacheza ndani ya Liverpool.
Salah alifunga kwenye mchezo dhidi ya Wolves wakati Liverpool iliposhinda mabao 3-1 na Son yeye alitupia mabao mawili wakati Tottenham iliposhinda mabao 5-0 Norwich City na timu yake imekata tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Salah amesema kuwa ni jambo kubwa ambalo amefanya mshambuliaji huyo anastahili pongezi kwa kuwa alikuwa akifanya vizuri kwenye kutimiza majukumu yake.
“Anastahili pongezi na amefanya kazi kubwa hivyo ninaweza kusema kwamba hongera kwake kwa kufanya kazi kubwa,”.