RIPOTI kutoka nchini Ujerumani zinadai kuwa Sadio Mane atawaaga wachezaji wenzake wa Liverpool baada ya mchezo wa fainali ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya kesho Mei 28, 2022 mchezo watakaocheza dhidi ya Real Madrid.
Mkataba wa Mane ndani ya Liverpool unaisha Juni 2023 na alipoulizwa juu ya hatma yake kama atasalia klabu hapo alisema ataweka wazi hatma yake baada ya mchezo wa fainali hapo leo.
Sadio Mane raia wa Senegal mwenye umri wa miaka 30 anahusishwa kujiunga na vilabu vya Bayern Munich ya nchini Ujerumani, FC Barcelona na Real Madrid zote za Hispania.
Na ada ya uhamisho ya mchezaji huyo inatajwa kuwa ni pauni million 25 ambayo ni zaidi Bilioni 73.