PABLO AWAPA KAZI MAALUMU MABEKI WAKE

KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco amefichua kuwa amewaonya mabeki wa timu hiyo, wakiwemo Henock Inonga na Joash Onyango kuongeza umakini juu ya washambuliaji wa Yanga wakiongozwa na Fiston Mayele.

Simba wanatarajia kucheza na Yanga katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA unaotarajia kupigwa Mei 28, mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza.

 Pablo amesema kuwa moja kati ya jambo la msingi kwa safu yake ya ulinzi kuhakikisha waharuhusu bao la mapema kutoka kwa washambuliaji wa Yanga katika mchezo huo.

“Najua haitokuwa mechi rahisi lakini tutafanya maandalizi ya kuweza kupata ushindi kwa sababu tunajua ukubwa na umuhimu wa mchezo wenyewe hivyo maandalizi yetu yatakuwa makubwa kulingana muda ambao upo kwa sasa.

“Matarajio yetu ni kuweza kushinda mchezo husika lakini lazima safu ya ulinzi isiruhusu bao la mapema kutoka kwa washambuliaji wa Yanga kwa sababu ukiangalia mchezo huu kutoka ni wa kushinda na kwenda hatua nyingine hivyo ndoto ya kila mmoja ndani ya timu kuweza kuifikia,” amesema Pablo.