8 BORA LIGI YA SOKA LA UFUKWENI KUANZA

LIGI Kuu ya Soka la Ufukweni inatarajiwa kuanza rasmi baada ya uchaguzi wa timu zilizoingia 8 bora kumalizika na mashindano hayo yataaza kufanyika Juni 10 katika Viwanja vya Coco Beach.

Katika hizo timu zilizochaguliwa 8 bora zimepangwa katika makundi mawili kila kundi lina timu nne na kwa siku zitachezwa mechi nne ili fainali iweze kufanyika mapema.

 Kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Soka la Ufukweni, Deogratius Lucas amesema kuwa kila kitu kinakwenda sawa na mipango ikikamilika taarifa itatolewa.

“Soka la ufukweni litakwenda kuaza Juni 10 na tayari timu zilizoingia hatua ya 8 bora zimechaguliwa  lakini hatuwezi kuzitaja kwa sasa mpaka pale uongozi utakapo maliza makubaliano yao na timu zilizoingia hatua hiyo”.

Mashindano hayo yanadhaminiwa na Global TV na Global Radio.