NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wataingia kwa tahadhari leo Uwanja wa CCM Kirumba kusaka ushindi mbele ya Biashara United.
Mchezo wa leo unatarajiwa kuchezwa saa 10:00 jioni ambapo timu zote zipo kwenye msako wa pointi tatu muhimu.
Yanga kwenye msimamo inaongoza ligi ikiwa na pointi zake 63 baada ya kucheza mechi 25 huku Biashara United ikiwa na pointi 23 baada ya kucheza mechi 24 ipo kwenye hatari ya kushuka daraja.
Nabi amesema:”Natambua kwamba Biashara United ni moja ya timu imara na zenye ushindani hivyo tutaingia uwanjani kwa tahadhari ili kuweza kupata pointi tatu muhimu,”.
Ikiwa Yanga itashinda leo itakuwa imenguza presha ya kuweza kuufikia ubingwa kwa kuwa itakuwa imebakiza mchezo mmoja tu ambao ikishinda itajihakikishia kutwaa ubingwa wa ligi ulio mikononi mwa Simba.
Mchezo uliopita Yanga ilishinda mabao 2-0 ilikuwa mbele ya Geita Gold na mtupiaji wao namba moja Fiston Mayele alitupia bao moja na kufikisha mabao 13.