Home Sports PABLO MAMBO MAGUMU NDANI YA SIMBA

PABLO MAMBO MAGUMU NDANI YA SIMBA

MAMBO magumu kwa Pablo Franco ndani ya kikosi cha Simba baada ya jana kulazimisha sare ya pili mfululizo kwenye ligi mbele ya Geita Gold baada ya mchezo uliopita kufungana bao 1-1 dhidi ya Azam FC.

Mastaa wake wakiwa Uwanja wa CCM Kirumba walikubali sare ya kufungana bao 1-1 kwenye mchezo wa ligi ambao ulikuwa wazi kwa timu zote na kuifanya Simba kufikisha pointi 51.

Mabao yote yalifungwa dakika 45 za mwanzo ulichezwa na iliwachukua dk 20 Geita Gold kufunga bao kupitia kwa mshambuliaji namba moja George Mpole akitumia makosa ya mabeki wa Simba waliokuwa wanaongozwa na Joash Onyango.

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 51 ikiwa tofauti na pointi 9 na Yanga iliyo nafasi ya pili na pointi 60 zote zimecheza mechi 25 na Yanga inabakisha pointi 5 kuweza kukabidhiwa ubingwa ambao ni sawa na mechi mbili Geita Gold wanafikisha pointi 35 wanabaki nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.

Bao alilofunga Mpole ni la 14 akimuacha kwa bao moja Fiston Mayele mwenye mabao 13 ndani ya Yanga liliweza kudumu dk 7 kwa kuwa Kibu Dennis alipachika bao dk ya 27.

Bao la Kibu mwenye rasta ni la 7 msimu huu ukiwa ni wa kwanza kucheza ndani ya timu hiyo akitokea Mbeya City yenye maskani yake Mbeya akiwa sawa na Meddie Kagere wa Simba.

Beno Kakolanya kipa ambaye alianza kwenye lango la Simba hakuwa na chaguo la kufanya baada ya shuti kali la Often Chikola dk ya 25 kumpita kwenye mikono yake na usalama wake liligonga besela na Beno kipindi cha pili alionyeshwa kadi moja ya njano.

Kapombe alikwama kuyeyusha dk 90 kwa kuwa aliumia na nafasi yake ilichukuliwa na Jimyssone Mwanuke ilikuwa dk ya 24.Pia John Bocco naye aliumia kwenye mchezo huo nafasi yake ilichukuliwa na Kagere dk ya 61.

Mastaa wengine wa Simba ambao walionyeshwa kadi ya njano ni pamoja na Onyango dk ya 28,Erasto Nyoni njano dk 90 huku kwa Geita Gold ni Yusuph Kagoma alionyeshwa kadi ya njano dk ya 64 na Edmund John ilikuwa dk ya 76.

Kiungo Pape Sakho alikuwa kwenye uangalizi mkali huku kipa namba moja Aishi Manula yeye alipata maumivu kwa kujikata na vioo kwenye vidole muda mfupi kabla ya mchezo.

Previous articleVIDEO:LICHA YA USHINDI WA 4-1,KIDAO ANAAMINI KAZI BADO
Next articleYANGA KUIKABILI BIASHARA UNITED KWA HESABU