HT:BIASHARA UNITED 0-0 YANGA

 DAKIKA 45 za mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Biashara United v Yanga zimemeguka Uwanja wa CCM Kirumba leo Mei 23.

Ubao unasoma Biashata United 0-0 Yanga ambapo kila timu inacheza kwa kushambulia na mpira wa pasi nyingi.

Yanga ambao ni vinara wa Ligi Kuu Bara wamepiga jumla ya kona mbili ambazo hazijaleta matunda huku Biashara United wakicheza kona moja.

Hakuna mchezaji ambaye ameonyeshwa kadi ya njano wala kuumizwa kutokana na migongano ya ndani ya uwanja.

Winga mshambuliaji wa Yanga, Dickosn Ambundo na mshambuliaji Fiston Mayele wamekuwa wakitengenezea nafasi kuliandama lango la Biashara.

Biashara United wao mchora ramani ni Ramadhan Chombo ambaye anatimiza majukumu yake.