TIMU ya Taifa ya Tanzania ya Wasichana chini ya miaka 17, Serengeti Girls, leo imefanya kweli kwa kupata ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Cameroon.
Ushindi huo muhimu ulikuwa ni kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa mtoano wa kuwania kusaka tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia uliokuwa na ushindani mkali ndani ya dk 90.
Nyota Clara Luvanga aliweza kufunga mabao matat huku moja likijazwa kimiani na Diana William kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Omnisport Ahmadou Ahidjo ulioko Yaounde.
Baada ya mchezo huo timu hiyo inatarajiwa kurejea Tanzania kwa ajili ya mchezo wa marudiano unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa,Juni 5 mwaka huu na mshindi wa jumla atafuzu kushiriki Kombe la Dunia nchini India mwaka huu Oktoba