KUMEKUCHA kwa wawakilishi wa Tanzania, Timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake, U 17 kuweza kuwakilisha nchi kwenye mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia.
Maandalizi ambayo walianza kuyafanya awali kabla ya mchezo inaonesha kulikuwa na mpango wa kupata ushindi kwenye mchezo ujao ambao utakuwa na ushindani mkubwa.
Kikubwa kwa vijana hawa ambao wanaiwakilisha Tanzania lazima wakubali kwamba wapo ugenini na wanakutana na timu ngumu.
Kushinda ugenini kwa Cameroon sio kitu kidogo hivyo ni lazima kwa wawakilishi hawa kutumia vema mbinu ambazo wamepewa.
Mchezo huu ni muhimu kwa kuwa yule anayeshinda anapiga hatua moja kuweza kufuzu Kombe la Dunia kwa kuwa malengo ya timu zote ni kuweza kupata tiketi ya kucheza Kombe la Dunia.
Kila la kheri kwa wawakilishi wetu na kwenye mchezo huo ambao utakuwa na ushindani mkubwa ni muhimu kujituma bila kuogopa kupata matokeo unaotarajiwa kuchezwa Mei 22,2022