HT:YANGA 3-0 MBEYA KWANZA

NDANI ya dakika 45, Yanga imefunga mabao 3-0 dhidi ya Mbeya Kwanza kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaochezwa Uwanja wa Mkapa.

Kasi walianza nayo ndani ya dakika 15 kwenye mchezo huo huku Mbeya Kwanza wakiwa kwenye mbinu ya kujilinda zaidi kwenye mchezo wa leo.

Ni mabao ya Fiston Mayele ambaye ametupia bao la kufungulia kwa Yanga dk ya 34 kisha msumari wa pili ni mali ya Said Ntibanzokiza ambaye alipachika bao dk ya 38.

Mwendo wa kwenda mapumziko umepelekwa na Dickon Ambundo ambaye amepachika bao hilo dk ya 45 mbele ya Mbeya Kwanza.