VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wanaonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi Ijumaa watakuwa kwenye msako wa pointi tatu.
Ni mchezo wa ligi dhidi ya Mbeya Kwanza utakaochezwa Uwanja wa Mkapa saa 1:00 usiku.
Awali mchezo huo ulitarajiwa kuchezwa Jumamosi ya Mei 21 sasa ngoma itapigwa Mei 20, Uwanja wa Mkapa.
Yanga imetoka kushinda mabao 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji na Mbeya Kwanza imetoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Geita Gold, Uwanja wa Majimaji,Songea.
Enock Jiah wa Mbeya Kwanza anatarajiwa kukosekana kwenye mchezo huo baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo uliopita dhidi ya Geita Gold.