SIMBA YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA AZAM FC

PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC unaotarajiwa kuchezwa kesho Mei 18 Uwanja wa Azam Complex.

Azam FC imetoka kupoteza mchezo wake wa ligi mbele ya Mbeya City kwa kufungwa mabao 2-1 Uwanja wa Sokoine, Mbeya, inakwenda kukutana na Simba ambayo imetoka kushinda mabao 2-0 Kagera Sugar.

Pablo ameweka wazi kwamba wapinzani wake wapo imara na anawaheshimu lakini atakwenda kujitahidi kushinda kwenye mchezo huo ambao ni Dabi ya Mzizima.

“Utakuwa ni mchezo mgumu na kila timu inahitaji ushinda hasa ukizingatia kwamba kila mmoja anahitaji pointi tatu muhimu kwenye mchezo wetu.

“Ambacho tunakwenda kufanya ni kwa wachezaji kujitahidi kutafuta ushindi hilo litawapa nguvu wachezaji wangu pamoja na mashabiki ambao wamekuwa wakijitokeza kwenye mechi zetu,”.

Huu unakuwa mzunguko wa pili kwa wababe hawa kukukutana uwanjani kwenye mechi ya ligi ambapo ule wa kwanza Azam FC ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1.