Home Sports AZAM FC WAANZA KUIWINDA SIMBA

AZAM FC WAANZA KUIWINDA SIMBA

ZAKARIA Thabit, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa kwa sasa wanafanya maandalizi kwa ajili ya mchezo wao ujao dhidi ya Simba.

Azam FC inakumbuka kwamba kwenye mchezo wao uliopita dhidi ya Simba ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 hivyo itakuwa kwenye kazi ya kusaka ushindi mbele ya wapinzani wao.

“Tulitoka Mbeya ambapo mchezo wetu ule umeshapita na sasa tumeanza maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya Simba ambao ni muhimu na tunahitaji matokeo.

“Kile ambacho kimepita benchi la ufundi litafanyia kazi na ambacho kwa sasa kimeanza ni maandalizi ya mchezo wetu ujao,Uwanja wa Azam Complex,” amesema.

Azam FC imetoka kupoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City inakwenda kukutana na Simba iliyotoka kushinda mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar.

Itakuwa ni Jumatano ya Mei 18,2022 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex.

Previous articleSAUTI:MAYELE KUTETEMA,NABI APIGA MKWARA
Next articleSIMBA YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA AZAM FC