STEVEN Gerrard, Kocha Mkuu wa Aston Villa amesema kuwa Jurgen Klopp anastahili kuendelea kukaa ndani ya Liverpool kwa miaka mingi kwani amefanya mambo makubwa.
Klopp bado yupo ndani ya Liverpool mpaka 2026 baada ya kuongeza kandarasi ya miaka miwili.
Mkataba wake wa awali ulikuwa unatarajiwa kumeguka mwaka 2024 hivyo bado yupoyupo sana ndani ya timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu England.
Kocha huyo amesema:”Anastahili kuwa hapo amefanya makubwa kazi kubwa ndiyo maana hata mashabiki wenyewe wamekubali hilo ameitengeneza timu hiyo na imekuwa ya daraja la juu,”.
Liverpool leo ina kazi ya kusaka shindi mbele ya Southampton ambao ni mchezo wa Ligi Kuu England.
Kwenye msimamo ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 86 baada ya kucheza mechi 36 vinara ni Manchester City wenye pointi 90.