SIMBA YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO

MABINGWA watetezi wa Kombe la Shirikisho,Simba wamefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kuweza kushinda mchezo wao leo mbele ya Pamba ya Mwanza.

 Uwanja wa Mkapa umesoma Simba 4-0 Pamba baada ya dakika 90 za nguvu kukamilika kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali.

Ni mabao ya Peter Banda dk 45,Kibu Dennis alitupia  dk 48 na Yusuph Mhilu huyu alitupia mabao mawili ilikuwa dk ya 53 na 90.

Ushindi huo unawafanya waweze kutinga hatua ya nusu fainali ambapo watakutana na Yanga iliyotangulia kushinda.

Yanga ilishinda mbele ya Geita Gold kwenye mchezo wa robo fainali uliochezwa Uwanja wa Mkapa.