VIDEO:YANGA YAFUNGUKIA ISHU YA PENALTI YA MAYELE

HAJI Manara, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wakati uliopo kwa sasa ni mashabaki kuendelea kuwa bega kwa bega na timu hiyo na kuacha kujadili suala la mchezaji wao Fiston Mayele kukosa penalti mbele ya Tanzania Prisons kwa kuwa wanaamini kwamba ni jambo la kawaida kutokea kwenye mchezo.

Ameweka wazi kwamba Mayele ni mpigaji mzuri wa penalti hivyo hawana mashaka naye na pia kazi kubwa ni kusaka ushindi kwenye mechi ambazo zimebaki ili kuweza kufikia lengo la kutwaa ubingwa wa ligi.