PABLO:KIPINDI CHA PILI NILIKUJA NA MBINU TOFAUTI

PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kwenye mchezo wake dhidi ya Kagera Sugar kipindi cha pili aliamua kwenda na mfumo tofauti kwa kuwa walipata ushindi wa mapema.

Mei 11, Uwanja wa Mkapa, Simba iliweza kushinda mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar na mabao yalitupiwa na Kibu Dennis dk ya 14 na John Bocco dk ya 30.

Kwa upande wa Kagera Sugar kipindi cha kwanza Uwanja wa Mkapa walionekana kucheza kwa kujilinda huku wakikosa nafasi walizotengeneza na kipindi cha pili walikuja kwa mtindo wa kipekee.

Akizungumza na Saleh Jembe, Pablo amesema kuwa hakuwa na namna nyingine ya kufanya zaidi ya kubaduii mbinu kwa wachezaji wake kucheza mbele ya Kagera Sugar.

“Kipindi cha kwanza tulipata ushindi wa mapema hilo lilikuwa jambo la kwanza na kipindi cha pili niliwaambia kwamba wanapaswa wapate muda wa kupumzika na kucheza kwa umakini.

“Ilikuwa ni ngumu hasa ukizingatia kwamba hakukuwa na viungo wa asili kwenye eneo la ukabaji pamoja  na wale wa kutengeneza nafasi hivyo ilibidi nije kwa mtindo wa kipee na tumeshinda mchezo wetu,” amesema.

Simba inafikisha pointi 49 ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.