KIBWANA Shomari, beki wa Yanga amesema kuwa anafurahia kuwa ndani ya kikosi cha Yanga na ana imani ya kuendelea kufanya vizuri baada ya kuongeza mkataba wa miaka miwili.
Mkataba wa beki huyo chaguo la kwanza la Kocha Nasreddine Nabi ulikuwa unakaribia kufika ukingoni mwa msimu huu hivyo bado yupo sana ndani ya kikosi cha Yanga.
Ni pasi moja ya bao ametoa kati ya mabao 35 ambayo yamefungwa na timu hiyo kwenye mechi za ligi ambapo Yanga inaongoza ikiwa na pointi zake 57 baada ya kucheza mechi 23.
Kibwana amesema:”Nipo ndani ya Yanga kwa sasa na hii ni habari nzuri kwa wengi ambao wanapenda mimi kuwa hapa kwa Wananchi kuendelea kufanya kazi.
“Kwa wale ambao hawapendi nina amini kwamba itawauma basi wakae kimya na kwa sasa nipo ndani ya Yanga kama Wananchi wamenitaka mimi nani niweze kukataa kusaini Yanga?
Mei 10 Yanga walitoa taarifa rasmi kuhusu nyota huyo kuongeza mkataba wa miaka miwili kuweza kuendelea kuitumikia timu hiyo.