RASMI BEKI ALIYEWAPA TABU SIMBA ASAINI MIAKA MIWILI YANGA

KIBWANA Shomari, beki wa kikosi cha Yanga ambaye aliwapa tabu watani zao wa jadi Simba mechi zote mbili msimu huu kwenye ligi ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza, Kibwana alikula sahani moja na Bernard Morrison ambaye alikwama kuifunga Yanga na mchezo wa pili alipopewa Pape Sakho na Bernard Morrison wote walikwama kufurukuta mbele yake.

Beki huyo ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi na mkataba wake ulikuwa unakaribia ukingoni mwishoni mwa msimu huu.

Beki huyo amesema kuwa habari ambayo anatoa ni mbaya kwa wasiopenda na kwa wale ambao wataipenda itakuwa nzuri kwao kwa kuwa ameshaongeza mkataba wa miaka miwili.

Kibwana alijiunga na Yanga akitokea kikosi cha Mtibwa Sugar na sasa yupo na Dicson Job ambaye walikuwa naye ndani ya Mtibwa Sugar.

“Habari nzuri kwa watakaoipenda na wale ambao hawataipenda itakuwa mbaya kwao nimeongeza mkataba wa miaka miwili, Wananchi wenyewe wametaka mimi ni nani nisikubali,?