GUADIOLA:TUMESHINDA LAKINI WATU WANAIPENDA LIVERPOOL

PEP Guardiola, Kocha Mkuu wa Manchester City amesema kuwa amepata pointi tatu lakini anaamini kwamba watu wengi hawapendi.

Manchester City iliwatungua mabao 5-0 Newcastel United kwenye mchezo wa Ligi Kuu Engand uliochezwa Uwanja wa City Of Manchester.

Raheem Sterling alifunga mabao mawili ilikuwa dk 19,90+3,Aymeric Laporte alitupia dk ya 38,Rodri dk 61 na Phil Foden dk 90.

Kocha huyo amesema:”Kila mmoja kwenye nchi hii anaipenda Liverpool,mpaka kwenye vyombo vya habari pia kila mmoja anaipenda Liverpool,” amesema Guardiola.

“Hiyo ni kweli kwa sababu Liverpool ina historia nzuri katika masuala ya ushindani Ulaya sio kwenye Ligi Kuu England tu kwa kuwa wameweza kushinda taji moja baada ya miaka 30,”

Kwenye msimamo Liverpool ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 83 na City inaongoza ikiwa na pointi 86.