KLABU ya DTB imefanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 mbele ya Pamba FC na wameweza kupata nafasi ya kupanda moja kwa moja Ligi Kuu Tanzania Bara.
Jumla wamefikisha pointi 65 baada ya kucheza mechi 28 ndani ya Championship msimu huu.
Pamba FC inabakiwa na pointi zake 36 baada ya kucheza mechi 28 msimu huu wa 2021/22.
Licha ya Pan African kushinda bao 1-0 dhidi ya Mwadui FC bado imekuwa kwenye nafasi ngumu ya kuweza kujinasua kutoka kwenye hatari ya kushuka daraja.
Kibindoni ina pointi 21 baada ya kucheza mechi 28 na Mwadui FC ipo nafasi ya 15 na ina pointi 23 zipo kwenye hatari ya kushuka daraja.