LEO Jumapili ya Mei 8,2022 Simba ikitarajiwa kucheza dhidi ya Ruvu Shooting, inatarajiwa kuwakosa Clatous Chama na Sadio Kanoute ambao ni majeruhi.
Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu ameweka wazi kwamba nyota hao hawapo fiti kutokana na kusumbuliwa na majeraha.
“Tuna majeruhi wawili ambao hawatacheza mechi yetu ambao ni Sadio Kanoute na Clatous Chama.”
Huu ni mchezo wa mzunguko wa pili kwa msimu wa 2021/22 Simba kumenyana na Ruvu Shooting ambapo ule wa awali ni mabao 3-1 Simba ilishinda.
Katika mechi iliyopita kwenye sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Namungo viungo hao wawili walikosa mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.
Chanzo:Spoti Xtra