SIMBA YATAJWA SARE ZA YANGA

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi sababu kubwa ya kupata sare katika michezo yao miwili mfululizo iliyopita ni uchovu ambao wachezaji wao walikuwa nao, kutokana na kutumia nguvu kubwa ya kujiandaa na kucheza mchezo wao wa Dabi ya Kariakoo dhidi ya Simba uliopigwa Jumapili iliyopita.

Aprili 30,2022wababe haowalikutana uwanjani kwenye mchezo wa ligi na kugawana pointi mojamoja baada ya ubao kusoma Yanga 0-0 Simba ikiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema: “Naweza kusema matokeo hayo kwa kiasi kikubwa yamechangiwa na uchovu waliokuwa nao wachezaji kutokana na maandalizi na kucheza mchezo wetu dhidi ya Simba.

“Lakini jambo zuri kwetu ni kuwa bado tunasalia kileleni mwa msimamo na tuliwapa mapumziko mafupi wachezaji, naamini tutarejea tukiwa bora zaidi kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons.”

Mchezo wa pili kwa Yanga kupata sare ilikuwa mbele ya Ruvu Shooting uliochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika,Kigoma.