AZAM FC YAIMALIZA KMC,YAKWEA PIPA

BAADA ya ushindi wa mabao 2-1 ambayo waliyapata jana Mei 7,2022 kwenye mchezo wa ligi dhidi ya KMC leo Mei 8 kikosi cha Azam FC kimekwea pipa kuelekea Mbeya.

Mabao mawili ya Rodgers Kola yalitosha kuipa pointi tatu Azam FC kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Kwa KMC ni bao la nyota Miraji Athuman ambaye alifunga bao hilo kipindi cha pili cha mchezo baada ya zile dakika 45 za kipindi cha kwanza kuwa mali ya Azam FC.

Azam FC inakwenda kukabiliana na Mbeya City kwenye mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sokoine.

Utakuwa ni mchezo wa 23 kwa Azam FC ambapo ule wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Azam Complex waligawana pointi mojamoja baada ya sare ya kufungana mabao 2-2.