NYOTA wa zamani wa Manchester United, Ramon Calliste ambaye alitamba utotoni na akina Cristiano Ronaldo na Wayne Rooney, ameliacha soka na kuwa muuza saa za kisasa.
Calliste alikuwa akitajwa kama Ryan Giggs ajaye, alitamba katika timu ya vijana ya United. Hata hivyo, jeraha baya la enka alilopata mwaka 2006, lilimlazimisha astaafu soka mapema.
Baadaye mwaka 2013, akafungua biashara yake ya kuuza saa jijini London, ambazo moja inaweza kupatikana hata kwa pauni 250,000 (milioni 726).
“Saa ilikuwa ni kitu ninachokipenda tangu zamani. Nilijifunza biashara hii haraka sana, nikavutiwa, na nashukuru tangu wakati huo biashara imeendelea kukua.”